Kiswahili | English |
Ukweli wa kufahamu kuhusu nimonia

Kifo kimoja katika vifo vitano vya watoto wa umri wa chini ya miaka 5 husababishwa na nimonia.

Kikohozi, mafua, kuwashwa koo na kutiririsha makamasi ni mambo ya kawadia katika maisha ya watoto. Kwa kawaida sio mambo ya kutisha. Hata hivyo, wakati mwingine kikohozi ni dalili mabaya ya ugonjwa hatari zaidi, kama vile nimonia au kifua kikuu.

Ugonjwa wa nimonia ndio unaoongoza ulimwenguni kwa kusababisha vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka 5, ukifuatiwa kwa karibu na ugonjwa wa kuhara. Watoto wote wa kike na wa kiume wana haki ya kupata huduma bora za afya ili kuhakikisha kwamba maambukizo ya njia ya hewa na magonjwa mengine yanagundukika kwa usahihi na kutibiwa vizuri kabla hayajasababisha madhara.

Baadhi ya ukweli wa kufahamu kuhusu nimonia

  1. Mtoto mwenye ugonjwa wa kikohozi au mafua asiwekwe kwenye baridi na alishwe chakula na vimiminika vya kutosha.

  2. Wakati mwingine, kikohozi ni dalili ya tatizo baya. Mtoto anayepumua haraka haraka au kwa shida anaweza kuwa na nimonia, uambukizo katika mapafu. Huu ni ugonjwa hatari kwa maisha ya mtoto. Mtoto akiwa na hali hiyo anahitaji huduma ya haraka ya mtaalamu wa afya, ambaye anaweza pia kushauri apelekwe hospitali kubwa.

  3. Familia zinaweza kuzuia nimonia kwa kuhakikisha kwamba watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo na kwamba wanalishwa vizuri na wanapewa chanzo zote.

  4. Mtoto mwenye kikohozi cha muda mrefu kinachoendelea kwa zaidi ya wiki tatu anahitaji kupata matibabu haraka. Mtoto anaweza kuwa ana ugonjwa wa kifua kikuu au uambukizo kwenye mapafu.

  5. Watoto na mama wajawazito wanaokaa kwenye mazingira yenye moshi wa sigara au wa kuni wako katika hatari zaidi ya kuugua nimonia au magonjwa mengine ya njia ya hewa.

Mada inayofuata