Kiswahili | English |
Kuhusu

Nini maana ya “Ukweli kuhusu Maisha”?

Taarifa huweza kuokoa maisha, kuboresha afya na kupunguza mateso.

Taarifa huweza kuokoa maisha, kuboresha afya na kupunguza mateso. Taarifa husaidia kuongeza upeo kuhusu njia na gharama rahisi katika kukinga, kutibu na kuzuia magonjwai. Changamoto iliyoko ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo na ufahamu wa pamoja miongoni mwa wazazi, walezi na jamii: hatua ya kwanza muhimu katika mapambano ya kulinda watoto dhidi ya magonjwa na dhidi ya madhara mengine. Ukweli kuhusu Maisha hukupatia taarifa muhimu kuhusu namna ya kuzuia vifo, magonjwa, majeraha na ukatili kwa watoto na kwa mama mzazi . Jarida la Ukweli kuhusu Maisha limeandaliwa kwa pamoja na mashirika ya umoja wa Mataifa ya UNICEF, WHO, UNESCO, UNFPA, UNDP, UNAIDS, WFP na Benki ya Dunia.

Toleo hili la Ukweli kuhusu Maisha limetokana na marekebisho kidogo yaliyofanywa katika toleo la kwanza lililoandikwa kwa lugha rahisi na UNICEF DRC’s Digital Communication kwenye www.ponabana.com.

Ukweli kuhusu Maisha una lengo la kuipatia familia taarifa muhimu zinazohitajika katika kuokoa na kuboresha maisha ya watoto. Wazazi,babu/bibi, walezi wengine pamoja na vijana wanaweza kutumia chanzo hiki cha habari kupata majibu ya maswali yanayohuisiana na uzazi hasa kwa mara ya kwanza na huduma nzuri kwa watoto tangu pale wanapozaliwa. Changamoto iliyoko ni kuhakikisha kwamba kila mhusika anafahamu na kuelewa ukweli uliomo katika jarida hili na anakuwa tayari kuutumia ukweli huo katika maisha halisi.

Soma Ukweli wote kuhusu Maisha.